Saturday, May 31

Screen Shot 2014-05-31 at 2.22.49 AM 
Hii ni stori nyingine tena ya 2014 ambayo inaingia kwenye list ya zile stori ambazo ukishaisoma au kuipata unaanza kufikiria mara mbilimbili na kujaribu pia kutengeneza picha yako mwenyewe kama upo eneo la tukio.
Watu wa karibu wa Mtuhumiwa huyu walijitokeza Mahakamani ili kuangalia kama ndugu yao aitwae Simon Ngozi (21) ataweza kupata dhamana kwenye kesi inayomkabili ya kubaka mtoto wa miaka tisa.
Imetokea Kenya ambapo jamaa alikua amepelekwa Mahakamani Makadara Nairobi lakini ghafla akamshangaza kila mtu baada ya kutaka kumaka Mwanamke aliekua karibu yake baada ya kuanza kumshikashika.
Screen Shot 2014-05-31 at 2.41.44 AM
Nje ya Mahakama ya Italia
Mshukiwa huyu alikuwa kortini kujibu tuhuma za kumbaka mtoto wa miaka tisa April 2014 ambapo wakati anataka kumbaka Mwanamke huyu Mahakamani tena kwenye
10334287_440249426112525_9027795163405871859_n_d173d.jpg
10388683_440249359445865_273072608345965805_n_f73c2.jpg


Mkulima mmoja nchini China ametengeneza sanduku ambalo pia ni kama pikipiki.

Sanduku hilo lina matairi mawili, na linaweza kubeba watu wawili, na linaweza kwenda umbali wa kilomita 60 kwa kasi ya kilomita 20 kwa saa. Linatumia nishati ya betri. Mkulima huyo He Liang ametumia miaka 10 kuunda sanduku hili. Lina nafasi ya kutosha kuweka nguo na likiwa tupu lina uzito wa kilo 7.


TYSON
Jana usiku habari zilizoshtua watu wengi ni kuhusu kifo cha director mashuhuri George Tyson. Hivi sasa kuna taarifa ambazo hazijawahi kutolewa na hawa wahusika kuhusu marehemu Tyson.
Zipo tano hadi sasa na zinatoka kwa watu mashuhuri kwenye kiwanda cha burudani. J1
Jokate Mwegelo amesema kuhusu kazi nzuri aliyokuwa anafanya George Tyson kama director wa The One show ambayo inaruka kupitia TV1
J2
Venessa Mdee hajawai kusema sababu ya kuacha kufanya The One show ambayo alianza hadi ku-shoot. Hivi sasa amesema sababu hiyo akimhusisha George Tyson kama mtu aliyempa moyo kwenye maamuzi yake.

 
 Pichani ni Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Morogoro Bw. Antony Mtaka akiwa na raisi wa wasanii Mwakifamba wakiingia eneo la Mochwari tayari kwa maandalizi yote kuwa sawa.
Mtangazaji na Muanzilishi wa Kipindi cha The Mboni Show, Mbonie Masimba akifutwa machozi mara baada ya kukaa na ndugu jamaa na marafiki, haamini

Tuesday, May 27

TZA NDOA YA SIKU 13 
Inaweza kuingia kwenye headlines kama tukihusisha countdown ya ndoa zilizodumu kwa muda mfupi tena zikifungwa kwa baraka zote kuanzia kwa wazazi hadi kanisani ambapo Bonface Oduor ambaye ndiye bwana harusi amesema >>‘alinisaliti baada ya siku 13 ya harusi yetu iliyofanyika weekend ya pasaka’
Bonface Oduor alimfumania mkewe akishiriki tendo la ndoa na mwanaume mwingine ikiwa ni siku 13 tu baada ya harusi yao ambapo alimkuta hotelini jijini Nairobi Kenya.
malaria
Damu kutoka kwenye kundi moja la watoto wa kitanzania iliyogundulika kuwa na kinga ya asili dhidi ya Malaria, sasa inawasaidia wanasayansi hao kutoka nchini Uingereza  kutengeneza chanjo madhubuti ya ugonjwa huo.hatari duniani.
Wanasayansi hao walikusanya sampo za kawaida za damu kwa watoto 1000 kutoka nchini Tanzania na kugundua kuwa damu ya takribani watoto sita kati ya 100 ina uwezo wa kupambana na vimelea vya Malaria.
malaria2
Watafiti hao kutoka chuo kikuu cha tiba cha Brown wamegundua kuwa
Mystery_MH370-747882
Hatimaye serikali ya Malaysia imeachia hadharani data halisi zilizotumika kugundua kuwa ndege iliyopotea ya MH370 ilianguka Kusini mwa bahari ya Hindi.
Data hizo kwa mara ya kwanza zilionyeshwa kwa ndugu na jamaa za abiria waliokuwa ndani ya ndege ambao wamekuwa wakitaka uwazi zaidi kuhusu taarifa hizo kabla ya data hizo kuwekwa hadharani kwa vyombo vya habari.
Mwenyekiti wa Bongo Muvi, Steve Nyerere akilia kwa uchungu.
Huzuni tele ikiwa imetawala wasanii waliokuwa viwanja ya Leaders.
Bi. Mwenda akilia kwa uchungu.

Monday, May 26



 Nasra akiwa na mama anayemlea kwa sasa Josephin Joel kutoka kambi ya ya wazee ya Fungafunga iliopo mjini hapa, akiwa katika chumba cha ICU  hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro anakopatiwa matibabu baada ya kufichwa katika box kwa miaka 4 na mama yake mkubwa Mariam Said baada ya mama yake mzazi kufariki mwaka 2010.



 Hali ya Narsa kwa sasa imezidi kutengemaa ,kunawili na kuonekana kama mtoto mwenye nuru kama anavyoonekana tofauti na alivyookolewa kutoka katika box siku tano zilizopita hapo mama  huyo mlezi akimpatia chakula iana ya wali na samaki anaopendelea Nasra. 



 Hapo Nasra akiwa ameshika kikombe kwa mikono yake mwenyewe ilioonekana awali kutokuwa na nguvu baada ya kuomba maji ya kunywa..



Petter Mwita Mtetezi wa haki za watoto mkoa wa Morogoro akiwa na Nasra katika kitanda anacholala mtoto huyo kwenye wodi ya watoto katika hospitali ya Rufaa  ya mkoa wa Morogoro. alishukuru vyombo vya habari kwa kutoa habari zilizofanya Nasra kupatiwa misaada mbalimbali.
ndege
Taarifa ya picha kamili za Satelite kuhusu ndege ya Malaysia iliyopotea MH370 zitatolewa kesho kwa mujibu wa maafisa wa nchi hiyo.
Kaimu waziri wa usafirishaji wa Malaysia Hishammuddin Hussein ametoa taarifa kuhusu kutolewa data za ndege hiyo wakati akiwa anatembelea kampuni iliyopo katika uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur.
ndege2
Familia na ndugu wa abiria waliokuwemo ndani ya ndege hiyo iliyopotea mwezi Machi mwaka huu ikiwa imebeba watu 239
Screen Shot 2014-05-26 at 6.11.50 PM 
Unaambiwa shindano hili ambalo limekua likifanyika na kuhusisha Watanzania toka lilipoanza ambapo ni Mtanzania mmoja tu (Richard) ndio alichukua ushindi katika miaka yote hiyo ya ushiriki.
Ilizoeleka shindano huwa linaanza mwezi May lakini la mwaka huu 2014 kutokana na kombe la dunia, litaanza September 7 ikiwa ni season 9 ambapo time hii idadi ya nchi zinazoshiriki ni ileile ya nchi 14 ila kuna nchi moja imeondolewa.
Angola wameondolewa na sasa Rwanda wameingizwa kwa mara ya kwanza huku nchi nyingine zitakazoshiriki zikitajwa kuwa
Michael
Meneja wa aliyekuwa mfalme wa Pop duniani Michel Jackson alijaribu kumteka staa huyo kumuokoa kutokana na dawa za kulevya.
Meneja huyo Ron Weisner ambaye ndiye aliyekuwa akidhibiti taaluma na kipaji cha marehemu Michael tangu enzi za ujana wake alikuja na mpango wa kutaka kumuokoa mfalme huyo wa Pop katika kilele cha matatizo yake mwaka 2006 wakati aliporipotiwa kuanza kuathiriwa na dawa alizokuwa akitumia.
Michael_Jackson-600x450
Kwa mujibu wa wataalamu kutoka kitabu kipya cha Ron kiitwacho ‘Listen Out Loud’, Meneja huyo alipanga kujiingiza katika mpango huo na dada wa Michel, Toya Jackson kumrubuni staa huyo wa ‘Thriller’ wamuibe na kumpeleka
Nigeria
Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, mpango kwa ajili ya kuachiliwa kwa baadhi ya wanafunzi wa kike waliotekwa nyara nchini Nigeria unakaribia kufikiwa wakati serikali ya Nigeria ikiitisha mpango wa makubaliano.
Baadhi ya wasichana walitarajiwa kuachiwa huru kwa kubadilishana na wafungwa wa Boko Haram.
Kundi la Boko Haram limewateka zaidi ya wasichana 200 waliokuwa shuleni Aprili 14 mwaka huu na kuamsha hisia kali miongoni mwa watu wengi wakiwemo viongozi wakubwa

Thursday, May 22

Hivi karibuni mwanamke mmoja huko Nchini Nigeria aliuawa na wananchi walioamua kujichukulia sheria mkononi baada ya kumtuhumu kuwa anaiba watoto wa shule na kuwapeleka kusikojulikana. 
Mwanamke huyu ambaye jina lake halikupatikana mara moja, alianza kupigwa na baadaye wananchi hao wakamuua kwa kumchoma moto. 

2014FIFAWorldCuplogo2-FIFA
Zimebaki siku chache tu kabla kipyenga cha kuashiria kuanza rasmi kwa michuano ya Kombe La Dunia la Soka kwa mwaka 2014 zitakazofanyikia nchini Brazil hakijapulizwa. Jumla ya timu kutoka mataifa 32 zinatarajiwa kushuka dimbani kuwania kombe hilo ambalo mshindi hutambulika kama mwamba wa soka duniani.
Kombe la Dunia huwa ni mkusanyiko wa mataifa na wachezaji wanaoaminika kuwa bora kabisa duniani. Mechi ya kwanza itakayopigwa Juni 12 itakuwa kati ya wenyeji Brazil watakaoanza kwa kumenyana na Croatia katika jiji la Sao Paulo.
Kabla ya ufunguzi na kabla bendera hazijapandishwa katika milingoni na magari na kabla fulana au jezi za timu hazijavaliwa mitaani na katika viunga vya sehemu mbalimbali duniani,haya hapa ni mambo 95 zikiwemo takwimu, historia kumbukumbu na mengineyo ambayo yanahusiana na Fainali za Kombe La Dunia ambayo tungependa uyajue [au ujikumbushe] kuhusu michuano ya Kombe La Dunia.
  1. Mechi za Kombe la Dunia mwaka 2014 zitafanyikia katika miji au majiji 12 tofauti nchini Brazil
  2. Kikaragosi au mascot wa Kombe la Dunia mwaka 2014 anaitwa Fuleco.
  3. Kombe la Dunia mwaka huu 2014 linamaanisha kwamba hii ni mara ya 5 kwa fainali hizo kufanyikia katika bara la Amerika ya Kusini. Mara ya mwisho lilifanyikia barani humo nchini Argentina mwaka 1978.
  4. Mwaka 1998 Ufaransa walikuwa wenyeji wa fainali hizo kwa mara ya pili.Mara ya kwanza walikuwa wenyeji mwaka 1938.

Mwimbaji mahiri nchini aliyefariki dunia wiki iliyopita huko Thailand, Amina Ngaluma.

 MWILI wa mwimbaji mahiri nchini aliyefariki dunia wiki iliyopita nchini Thailand, Amina Ngaluma ‘Japanese’ unatarajiwa kuwasili Dar es Salaam Ijumaa wiki hii.
Kwa mujibu wa mume wa marehemu, Rashid Sumuni tayari taratibu muhimu kuhusiana na kuuleta mwili huo nyumbani zimefanyika na wana amini mambo yataenda kama wanavyotarajia.
“Naomba niwajulishe kuwa mwili wa mke wangu utaondoka Thailand Alhamisi wiki hii kwa ndege ya KLM na utawasili Dar es Salaam siku inayofuata saa tatu usiku.
“Tunaamini kama mambo yataenda kama tulivyopanga baada ya mwili kuwasili basi Jumamosi tutamhifadhi mwenzetu. Msiba upo kwa wazazi wa marehemu Kitunda, Machimbo, Dar es Salaam ambako ndiko maziko yatafanyika.
“Kimsingi imekuwa ngumu kusema tutazika lini, kwa sababu bado mwili haujaletwa, lakini tayari familia kwa kushirikiana na sehemu alikokuwa anafanya kazi na Watanzania wengine waishio kule tumeshamaliza taratibu zote zilizokuwa zikihitajika ili kuuleta mwili nchini,” alisema Sumuni kwa masikitiko.
Pia alivishukuru vyombo vya habari kwa kuwa karibu na familia yao wakati wa kipindi hiki kigumu, lakini akiomba wanapotaka kutoa habari kuhusiana na msiba huo wawasiliane na wahusika wa familia ili kupata taarifa
Huyu si mwingine bali ni Sheila Vogel-Coupe, miaka 85 raia wa
Screen Shot 2014-05-21 at 10.50.47 AM 
Ripota wa nguvu Simon Simalenga akiwa  Dodoma amekutana na Wanachuo kwenye chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) ambapo kwenye bunge la bajeti linaloendelea May 19 2014 Wabunge walipitisha bajeti ya wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi ambayo ni Bilioni 799.2
Ndani ya saa 24 toka kupitishwa kwa bajeti hiyo taarifa zinapatikana kwamba kuna uwezekano wa kutokea maandamano ya Wanachuo wa chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) kuelekea bungeni kama hawatopata fedha zao za kujikimu ambazo wamecheleweshewa kwenye collage yao ya Humanities.
Wanasema ‘hatujazungumza hivi sababu tumepanic, kikawaida chuoni tunatakiwa kusaini boom kila baada ya siku 56 ambazo ziliisha 26 April 2014 na mpaka hatujapata taarifa yoyote toka wakati huo kwamba kuna shida gani imetokea’
Mwajuma Ally ambae ni Mwanachuo wa UDOM pia amesema ‘niko mwaka wa pili, tunashindwa kuelewa kwa nini hili tatizo limetokea mpaka sasa hivi inaonekana sisi tunadharaulika manake hii ni mara ya pili inatokea humanities lakini vyuo vingine wamepewa mikopo’
 image_4
Baba mzazi wa flaviana pamoja na wadogo zake
Tanzania leo tumewakumbuka ndugu zetu ambao walipoteza maisha kwenye ajali ya kuzama kwa meli ya Mv Bukoba ambayo ilizama siku kama ya leo mwaka 1996 ambapo miongoni mwa watu waliopoteza maisha ni mama mzazi wa mwanamitindo Flaviana Matata pamoja na mtoto wa mjomba wake ambao walikua safarini.
Leo Flaviana Matata akiwa na Ambwene Yesaya ‘Ay’ na baadhi ya wasanii wengine wa Tanzania pamoja na viongozi mbalimbali wa dini waliungana na Watanzania waliopata nafasi kuhudhuria ibada iliyofanyika kwenye makaburi yaliyopo eneo la Igoma Jijini Mwanza.
image_11
image_10
image_5
 michael-jace-and-wife
Aliyekuwa staa ya series maarufu ya The Shield, Michael Jace ametiwa mbaroni kwa kosa la kumuua mke wake. Staa huyo alijisalimisha polisi baada ya kumuua kwa kumpiga risasi  aliyekua mke wake, April Jace, imerepotiwa.
Muigizaji huyo mwenye umri wa miaka 48 alikiri kumpiga mke wake risasi mara kadhaa baada ya ugomvi mkubwa uliotokea pale mke wake April, aliporudi nyumbani. April alikua anarudi na watoto baada ya kuwachukua kutoka kwenye mazoezi ya kikapo.
Imesemekana kua muigizaji huyo alikua na hasira juu ya matumizi ya pesa aliokua akifanya mke wake licha ya hali yao ya kifedha kua mbaya. Imeripotiwa kua hali yao

Tuesday, May 20

                   b3kuambianaKwa sasa kutoka hapa Leaders ni watu mbalimbali wanatoa heshima zao za mwisho wakiwemo waigizaji mbalimbali ambao marehemu Adam Kuambiana aliwahi kufanya nao kazi na wengine ambao hawakuwahi kufanya nae kazi,kwa mujibu wa ratiba iliyotangazwa mazishi yanategemewa kufanyika saa 9 kwenye makaburi ya Kinondoni.
Miongoni mwa watu waliokuwa na simanzi zaidi mpaka wakashindwa kuongea ni Jb hakumalizia kuongea 
 akawa anataka kudondoka chini

,18kuambiana

Bn_QOpaCEAAStDr  Jarida la Vogue la Marekani mwezi uliopita liliwatoa kwenye cover wapenzi wanaotarajiwa kufunga ndoa hivi karibuni Kim Kardashian na Kanye West, na mauzo ya jarida hilo yakawavunja rekodi ya cover za nyuma za jarida hilo, baada ya mafanikio hayo inaonekana Vogue sasa wamenogewa.
Jarida la Vogue lakini safari hii la Hispania limeamua kujibu mapigo ya wenzao wa US kwa kuwaweka kwenye cover mwanasoka bora wa dunia Cristiano Ronaldo na mchumba wake mwanamitindo Irina Shayk.

Changamoto ya mapungufu yaliyotajwa kwenye maandalizi ya vitabu na mitihani ya kumaliza darasa la saba imepelekea mheshimiwa James Mbatia kuwa-challenge maprofesa walioko bungeni kuufanya mtihani wa darasa la saba ambao kwa mujibu wake haufanyiki.
Akitoa mchango wake bungeni wakati wa mjadala kuhusu bajeti ya wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi ya mwaka 2014/2015, Mbatia amesema alichukua mtihani wa darasa la saba na kuupeleka kwa professor wa chuo kikuu cha Dar es Salaam na alimrudishia majibu kuwa mtihani ule haufanyiki.

“Njoo kwenye mtihani wa hisabati, na mimi napenda sana hisabati. Mheshimiwa spika, nilipeleka mtihani huu kwa professor wa chuo kikuu cha Dar es Salaam, mtihani wa darasa la saba. Professor ameniandikia hapa ‘nimetumia muda wa  saa mbili na dakika tatu kufanya mtihani huu bila kuandika majibu kwenye karatasi na mtihani wenyewe haufanyiki.  

"Yaani ni madudu matupu yako kwenye mtihani huu. Nawachallenge wenzangu ambao ni maprofesa na wengine wanajua hisabati, wafanye mtihani huu waweze kupata 100/1000 na mimi ntawapa shilingi milioni 10 ndani ya bunge hili.” Amesema James Mbatia.
Mwili wa Adam Kuambiana ukiandaliwa tayari kwa kuagwa nyumbani kwake Bunju B jioni hii.



Waombolezaji wakiwa msibani tayari kuaga mwili. Wa tatu kutoka kulia waliokaa mbele ni mke wa marehemu Janeth Rithe ambaye ni Diwani Kata ya Kunduchi, Dar.
prezdaa 
Nikikupa nafasi ya kuniambia namba ngapi atakua anacheza huyu president wa nchi kwenye hili soka unaweza kuotea?
prezzz 
Sasa unaambiwa club moja huko Bolivia (Sports Boys) imemsajili rais wa Bolivia Evo Morales kucheza kama kiungo wa kati kuanzia Agosti 2014 na mgongoni atakua na jezi namba 10 huku mshahara wake kwa mwezi ukiwa ni dola za Kimarekani 213 kwa mwezi ambazo ni zaidi ya laki 3 za Kitanzania.
Msanii wa muziki wa Bongo Flavour kutoka Tanzania Diamond Platnumz.
Msanii wa muziki wa Bongo Flavour kutoka Tanzania Diamond Platnumz.
Msanii wa muziki wa Bongo Flavour kutoka Tanzania Diamond Platnumz amekuwa akiongoza katika upigari kura wa kuwania tuzo za Muziki wa Televisheni ya Watu Weusi Marekani (Black Entertainment Television-BET) katika kipengele cha Best International Act: Africa.

Tuzo hizo zitatolewa jijini Los Angeles, Marekani Juni 29.
Mpaka jioni hii Diamond alikuwa anaongoza kwa asilimia 75.79.




Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam



Tukiwa bado na Majonzi ya Kifo cha Adam Kuambiana,msanii mwingine afariki Dunia leo Hospitali ya Taifa Muhimbili

II wa filamu hapa nchini, Adam Kuambi
ana, pichani juu, anatarajiwa kuzikwa keshokutwa Jumanne katika Makaburi ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, huku mazishi yake yakitanguliwa na shughuli ya kumuaga katika Viwanja vya Leaders Club, saa 2 kamili asubuhi.



Akizungumza leo mchana, jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Maafa na Sherehe wa Chama Cha Waigizaji mkoani Dar es Salaam, Kaftany Masoud, alisema taratibu za mazishi yake zitaanza kwa kuagwa Leaders Club.



Katika hatua nyingine, msanii wa maigizo na filamu, anayejulikana kwa jina la
20140519-205430-75270957.jpg
Wakati Manchester United wakifanya uteuzi wa kocha, Barcelona nao waliopoteza taji msimu huu sawa na Man U wamemteua Luis Enrique kuwa kocha wa kikosi chao cha kwanza.
Enrique (44) aliyepewa mkataba wa miaka miwili kuchukua nafasi ya Gerardo Martino ‘Tata’ aliyejiuzulu baada ya kukosa ubingwa, alikuwa kocha wa timu ‘B’ ya Barca tangu 2008 hadi 2011alipokwenda kuwafundisha Celta Vigo mpaka wiki jana.
Barca walishindwa kutetea ubingwa wao kwa kutowafunga Atletico Madrid wikiendi hii kwenye moja ya mechi za mwisho za La Liga na pia walitolewa kwneye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya huku wakishuhudia Atletico na Real Madrid wakiingia fainali inayochezwa wikiendi ijayo.
-