Maajabu! Mchungaji wa Kanisa la Pentecostal Spirit and Truth, Amani
Rubeni Mirumbe ameushangaza ulimwengu kwa kujitabiria kifo na baadaye
kufariki dunia kweli huku akiwaachia waumini na familia yake wosia wenye
viashiria vya kuzikwa Kiislam, Amani linakujuza.
Mwili wa mchungaji Amani Rubeni Mirumbe ukiagwa.
Kifo hicho kilijiri saa 3:12 asubuhi ya Machi 24, mwaka huu, Mabibo
jijini Dar es Salaam mahali lilipo kanisa na nyumba ya mchungaji huyo na
kuzikwa saa 10:21 jioni. Kwa maana hiyo, mwili huo ulikaa kwa saa saba
tu.
KILICHOSABABISHA KIFO
Saa chache baada ya kifo, Amani lilifika msibani na kufanikiwa kubaini mawili matatu kuhusu kifo cha mtumishi huyo wa Mungu.
Kwa mujibu wa mmoja wa waumini wake, marehemu Mchungaji Mirumbe alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya presha lakini asubuhi ya siku ya tukio, alipoamka alimwita msaidizi wake na kumwambia siku hiyo haiwezi kupita bila yeye kukata roho.
“Ni ajabu sana, alipoamka tu alimwita msaidizi wake, akamwambia siku ya leo (Jumatatu) lazima afe ila kabla ya kuiacha dunia anataka kuacha wosia wake kwa ajili ya familia na sisi waumini,” alisema muumini mmoja ambaye aliomba hifadhi ya jina.
WOSIA NI HUU
Muumini huyo alisema kuwa, mchungaji huyo akiwa katika hatua za mwishomwisho kabla ya kifo, aliacha wosia kwamba, akishakata roho hatataka mwili wake uzikwe ukiwa ndani ya jeneza kama wafanyanyiwavyo Wakristo au wachungaji wengine.

Ndugu wa mchungaji Amani Rubeni Mirumbe wakiomboleza kwa simanzi kubwa
“Marehemu aliagiza mwili wake uwekwe kwenye sanda na hata kama
ataagwa zoezi hilo lifanyike mwili ukiwa ndani ya s