Sunday, September 22

NAAM tumekutana tena kwenye kona ya mahaba ili kujuzana machache, hali yangu ni buheri wa afya sijui ninyi wenzangu. Kama ilivyo ada tunaendelea na mada nyingine ili tujue tumejikwaa wapi na wapi tuelekee.
Leo najua una hamu ya kujua nimekuja na mada gani, kwa vile madhumuni makubwa ya kona hii ni kukumbushana na kurekebishana hasa pale mtu anapokuwa amekwenda kinyume kwa kujisahau au kwa kutojua.

Katika mada ya leo nitazungumzia suala la kujipamba kwa wanaume kupita kiasi, si jambo geni kwa wanaume kujipamba ili waonekane maridadi mbele ya macho ya watu. Kama kutumia manukato ya kunukia na mafuta ya kulainisha ngozi.
Lazima tukubali mapambo ya mwanamke yana tofauti hata jinsi ya kujipamba ina tofauti kubwa. Lakini kumezuka mtindo wa kuiga kila kitu bila kuangalia mila na destuli zetu.

Kwa sasa imekuwa kazi kubwa kumtambua mara moja mwanamke au mwanaume kutokana na wanaume hasa vijana kuvamia mapambo ya kike.
Sasa hivi vijana wanajipaka mikorogo kutoga masikio zaidi ya tundu tatu, kusuka nywele kutoga midomo hata ulimi. Unajiuliza tatizo nini kipi kimepungua katika uanaume wako mpaka kujifananisha na mwanamke, unaamini kabisa wanaume wenye tabia hizo toka awali ni mashoga.

Kwa nini ifikie hatua watu wakufikirie vibaya kutokana na kujipamba kwako? Je utamaduni huo umeurithi toka wapi? Baba au babu yako amefanya hivyo?. Ni vitu ambavyo naweza kusema wazazi wamekuwa ndiyo chanzo cha mmomonyoko wa maadili kwa kuacha tatizo kuota mizizi.
Sawa zipo kabila ambazo zina utaratibu wa wanaume kusuka, wanawake kunyoa au wanaume kutoga masikio. hizo ndizo mila na destuli zao hakuna wa kuwashangaa. Leo hii kila kijana ambaye anaimba muziki wa kisasa mavazi yake na jinsi anavyojiweka ni tofauti na mila na destuli zetu.

Ajabu wazazi jambo lile wanalifumbia macho na wao kuona jambo la kawaida, nafikili ifike hatua wazazi wakubali kuwa wao ndiyo chanzo cha yote yanayoporomosha maadili yetu.
Napenda kuwaeleza vijana wote hata watu wazima ambao hutamani kila akifanyacho mwanamke na wao kufanya, ipo siku watavutiwa na kukuza matiti ili waende sambamba na mwanamke.
Lazima iwepo tofauti kati ya mwanamke na mwanaume katika mavazi, mapambo na pia muonekano. Tunajua mwanamke ni ua la dunia ameletwa ili kuipamba dunia na mwanaume ni kiongozi wake. Pia mwanamke anatakiwa kujipamba ili kumvuta mwanaume kama ua zuri kwa nyuki.

Leo hii mwanaume unajipamba ukisimamishwa na mwanamke kutofautisha inakuwa kazi. Unajipamba kama mwanamke una ajenda gani? Bado hujachelewa jiweke kama mwanaume ambaye akisimamishwa mbele ya wanaume akubalike, siyo watu wawe na mashaka na wewe.
Mfano mzuri ni kwa mzazi wako muangalie baba yako alivyo, Je anafanana na wewe unavyojiweka. Upende uanaume ili kuwa mwanaume kamili. Tuache kuiga bila kujua faida na hasara.

Kwa hayo machache tukutane kesho

Friday, September 20

Ni Jumatano nyingine tena tunakutana katika safu yetu nzuri ya kubadilishana mawazo juu ya uhusiano na wapenzi wetu. Ni imani yangu kwamba utakuwa mzima wa afya njema huku gurudumu la maisha likisonga kama kawaida.

Rafiki zangu wapenzi, Jumatano ya wiki iliyopita, nilipokea simu kutoka kwa msomaji mmoja usiku sana. Alisema aliguswa sana na mada zangu hasa ya siku ile, lakini alikuwa na matatizo ambayo alihitaji kupatiwa ushauri.

Katika mazungumzo nami, msomaji wangu huyo ambaye ni mwanamke (nitaficha jina lake) alisema yupo kwenye uhusiano na mwanaume ambaye kwake ni kero. Alisema, mpenzi wake huyo ana umri wa zaidi ya miaka 45 na yeye ana miaka 34, wakiwa katika uhusiano huo kwa zaidi ya miaka mitatu sasa.

Hata hivyo, alisema tatizo kubwa linaloyumbisha uhusiano wao ni kitendo cha mwanaume huyo, kuwa na tabia za kuwatongoza wadogo zake (wa kike) ambao anaishi nao nyumbani kwake. Baada ya kero hizo kuzidi, dada huyo aliona ni bora kuachana naye. Akamweleza mwanaume huyo msimamo wake na kuachana.

Kilichomfaya anipigie simu ni juu ya mwanaume huyo kumsumbua kila wakati, akitaka warudiane. Amekuwa akiomba msamaha na kuahidi kwamba hatarudia tena. Alisema, hii siyo mara yake ya kwanza, kwani mara nyingi amekuwa akiwatongoza hata rafiki zake wa karibu na akishtukia mchezo, kazi yake imekuwa kuomba msamaha akiahidi kutorudia lakini baada ya muda, hadithi inabaki kuwa ile ile!

Kinachomuuma zaidi ni kwamba, amejikuta akimpenda sana mwanaume huyo na anashindwa kabisa kumuondoa kichwani mwake. Nilizungumza naye juu ya tatizo lake, lakini niliona yawezekana kabisa kuna wengine wengi wenye tatizo kama lake, lakini hawajui cha kufanya.

Dada na kaka zangu, hapa nitakupa njia madhubuti za kutumia ili uweze kukabiliana na tatizo hilo katika uhusiano wako.
Je, wewe ni mwanaume/mwanamke ambaye upo katika uhusiano na mpenzi ambaye haishi kuwatongoza rafiki, ndugu au watu wako wa karibu? Vipengele vifuatavyo ni dawa tosha kwako...

ANAWEZA KUBADILIKA?
Siku zote katika uhusiano wowote ule, suala la msamaha ni jema na lenye nafasi kubwa ya kuboresha uhusiano, lakini kabla ya kuchukua hatua ya kusamehe ni lazima ujiulize, anaweza kubadilika?

Hili linaweza kuthibitishwa na historia yake ya nyuma. Haiwezekani ikawa ndiyo mara yake ya kwanza kukosea, lazima atakuwa ameshakukosea mara nyingie huko nyuma. Je, hili ni kosa lake la kwanza? Alivyokosea huko nyuma aliomba msamaha?
Kama aliomba, alirudia tena? Maana kama mtu anakosea kosa lile lile zaidi ya mara tatu na anaomba msamaha akiahidi kubadilika na habadiliki, ujue kwamba si rahisi kubadilika tena! Lazima ujiridhishe kwamba ni kweli atabadilika na hatarudia tena. Kama nilivyosema hapo juu, utapata ukweli huu kupitia historia yake ya nyuma!

MAKOSA NA UMRI
Rafiki zangu, kuna aina ya makosa fulani, ukishavuka umri fulani unakuwa huwezi kuyafanya tena, kwa mfano, kesi za kwenda disko na demu mwingine, kwa mwanaume wa miaka 45 huwezi kuzisikia tena. Sasa hata katika hili, lazima uangalie umri wake kama unafanana na kosa lake.

Unajua, kuna tabia nyingine hubadilishwa na wapenzi na nyingine ni za kuzaliwa ambazo kwa hakika huwezi kufanya mabadiliko. Suala la kubadilisha wapenzi, linaonekana kuwa fasheni zaidi kwa vijana, lakini kama umri wake umeshasonga na bado akawa na tabia hizo, ujue kwamba hiyo ni tabia yake ya asili ambayo haibadilishiki!

Mwanaume wa miaka 52 bado unakimbikizana na ‘vitoto’ vidogo, lazima kuna tatizo. Wataalamu wa Saikolojia ya Uhusiano na Mapenzi wanaamini wanaume wenye uwezo wa kuwa na familia bora na kuisimamia vyema ni wale wenye zaidi ya miaka 35, kwamba atakuwa ameshapitia mambo mengi na sasa anatamani kuwa baba tu! Msimamizi wa familia.

Fungua ubongo wako, msimamizi wa familia hawezi kuwa malaya, anatakiwa awe mwenye kujiheshimu. Huyu anafaaa? Wa nini? Akili kichwani mwako.
NI MWENZI SAHIHI?
Lakini pia, kabla hujachukua uamuzi wa kuachana naye, lazima ujiulize swali hilo hapo juu, ni mwenzi sahihi? Lazima awe na sifa zitakazomfanya apewe kofia ya mwenzi sahihi.

Rafiki zangu wapenzi, kutokana na ufinyu wa nafasi, naomba kuishia hapo kwa leo, nikikusihi usikose wiki ijayo katika sehemu ya mwisho ya mada hii ambapo nitafafanua sifa za mwenzi sahihi pamoja na suluhisho la mwisho la kukabiliana na tatizo hili.
Nakuacha na ujumbe mmoja muhimu zaidi, ni vyema kuwa makini sana na wenzi wetu, tuache kuamini na kusikiliza sana moyo, kwani wakati mwingine, huweza kukutumbukiza kwenye moto. Hata kama unampenda kiasi gani, lakini ana matatizo ambayo yanakulazimisha uachane naye. Kwanini unamng’ang’ania?

KESHO tutaendelea....

Thursday, September 19

Mkurugenzi wa mafunzo (AJTC) mwenye koti jeupe akiwa pamoja na baadhi ya wakufunzi wa chuo hicho wakisikiliza kwa makini moja ya mada za ujasiriamali zilizotolewa chuoni hapo hivi karibuni
 
 
·     Jumla ya wanachuo 227 wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha wanatarajiwa kushiriki katika mafunzo ya ujasiriamali na mbinu za ukuzaji wa biashara, yatakayotolewa na wakufunzi wa chuo hich
Baadhi ya wakufunzi wa AJTC wakifuatilia kwa makini semina ya ujasiriamili  iliyokuwa ikiendelea chuoni hapo


Akizungumza na blog hii mratibu wa mafunzo hayo Bwana Andrea Ngobole amesema kuwa: mafunzo hayo yatakuwa ya  siku mbili kuanzia tarehe 19-20/09/2013na  yanalenga kuwapa wanachuo hao juu ya  mbinu na maarifa  kuwa wajasiriamali na wafanyaiashara wenye mafanikio na kuwa chachu ya maendeleo kwa familia, jamii na taifa kwa ujumla

·       Amesema kuwa kitengo cha ujasiriamali chuoni hapo kimekuwa kikiandaa semina za ujasiriamali kwa wanachuo hao kila mwaka na kwa mwaka huu kinatarajia kuwasilisha mada 7 kutoka kwa watoa mada wanne ambao pia ni wakufunzi wa chuo hicho.

·       Semina hii itajumuisha mada kama Business Ventures, Business Networking na Business Family zitakazo wasilishwa na Neema Mwaipela pia kutakuwa na mada ya kutathimini biashara na misingi 10 ya ujasiriamali itakayowasilishwa na Ngobole pia Cash Flow Quadrant itakayowasilishwa na Adson Kagiye. Alisema Bw. Ngobole.

Wednesday, September 18

NAAM poleni na mihangaiko ya utafutaji wa riziki hata elimu, tumekutana tena kwenye mada mpya isemayo ‘Neno nakupenda linabeba vipi mapenzi?’. Hali yangu ni nzuri kwa uwezo wa Mungu na ninyi nina imani mu wazima wa afya njema.

Tuesday, September 17

                
ASSALAAM Alaykum/Bwana Asifiwe. Wiki iliyopita nilipokea maswali mengi kutoka kwa wasomaji wangu wa safu hii, wakiniuliza kuhusu hina, asmini, kilua na mrangiragi. Sikuweza kujibu kwa mtu mmoja mmoja lakini leo kupitia hapa, natoa majibu yote.ali ya

Monday, September 16

Tatizo la uwezo wa kufanya tendo la ndoa linazidi kukua miongoni wa wanandoa na wapenzi wengi. Takwimu za kitafiti zinaonyesha kuwa karibu ndoa 4 kati ya 10 zenye umri wa miaka 3 na kuendelea zinakabiliana na tatizo hili. Aidha wanaume 6 kati ya 10 wanatajwa kulalamikia upungufu wa nguvu za kiume na kuacha idadi ya wanawake wanaokabiliwa na tatizo hilo kwa mujibu wa uchunguzi kubaki na asilimia 13.

                            
                           
Baada  ya  video  wa  wanafunzi  wa  chuo/ college  flani  kunaswa  na  mtandao  huu   miezi  minne iliyopita, mpekuzi  wetu  amefanikiwa  kuinasa  video  nyingine  ya  wanafunzi  ambao  waliamua  kuigeuza HOSTEL  yao  kuwa  GESTI....

Friday, September 13



Mwanamke mmoja aliyebakwa alikuwa anaact kama anataka kumsamehe mwanaume aliyembaka miezi michache iliyopita akiwa amemtishia kisu.Mwanamke huyo aliamua kumkaribisha nyumbani kwake ili wafahamiane vizuri na pia wajadiliane maamuzi kuhusu kesi yao ya ubakaji nje ya maamuzi ya mahakama.

 Habari zilizokusanywa na Reportghananews.com zinasema kuwa,mwanaume huyo alipofika tu,mwanamke (aliyebakwa) alimpa sehemu ya kukaa alafu akamwambia kwamba anaenda kumwandalia chakula,ila alikuwa na kisasi akilini mwake.

Thursday, September 12



Utandawazi  umeendelea  kuwaangamiza  dada  zetu  wanaopenda  kuiga  mambo  wasiyoyajua....

Katika  mtandao  huu  umefanikiwa  kuzinasa  picha  za  mrembo  huyu akiwa  katika  pozi  la  nusu  uchi.

Saturday, September 7



Wapenzi ambao wapo katika uhusiano lakini hawajui mambo ya kufanya ili wawe bora kwa wapenzi wao. Mada hii itagusia pande mbili. Upande wa kwanza ni kwa wale ambao ndiyo kwanza wapo katika hatua za mwanzo kabisa na wapenzi wao na upande wa pili ni kwa wale ambao tayari wapo katika uhusiano lakini hawajui jinsi ya kuwafanya wawe bora kwa wapenzi wao.

                                            
 Daktari feki aliyenaswa katika hosptali ya KCMC aliyetambulika kwa jina la Alex Massawe akiwa amefungwa pingu mikononi mwake katika eneo la hosptali hiyo.
Mshike mshike wa maandalizi ya bonanza la 8 la vyombo vya habari maarufu kama media bonanza mkoa wa Arusha umepamba moto baada ya viongozi wa TASWA mkoa wa Arusha kutangaza zawadi kwa WASHINDI

                   
                                           

Thursday, September 5

                                
Wiki iliyopita tulianza somo hili lenye mada kuhusu dondoo zinazoweza kusaidia kuimarisha mapenzi, bila kupoteza muda tuendelee kutoka pale tulipoishia.

TENDO LA NDOA: Wataalamu wameandika mengi kuhusu umuhimu wa kutoshelezana kwenye tendo la ndoa, hivyo sipendi kueleza mengi lakini pengine nijazie kwa kusema kuwa

                                
Itanguruma jumapili hii ndani ya uwanja wa general tyre Njiro Arusha....USIKOSE WEWE MDAU!!!!!!!!!!!!!
                    

Tuesday, September 3




Pengine watu wengi wamekuwa wakitafuta ni jinsi  gani wanaweza kupendwa na wasichana au wanawake. Niwazi kabisa kila mwanamke anachaguo lake kwa mwanaume ampendae.Huenda ukawa unavigezo kibao lakini akapenda mweyevigezo vichache. Vifuatavyo ni vigezo 15 ambavyo wasichana wengi hupenda kutoka


Katika jitihada za kuhakikisha kuwa inawezekana kuweka kumbukumbu ya kila kitu kinachoendelea katika maisha ya binadamu masaa yote bila kupumzika kwa kutumia njia ya picha, Kampuni ya Memoto ya nchini Sweeden chini ya Martin Kaellstroem, wamefanikisha kutengeneza ki-camera kidogo ambacho huweza

BONYEZA LINK HII KUCHEKI MCHEZO HUO WA KUSTAAJABISHA

http://www.youtube.com/watch?feature=player_embedded&v=v4kVe1OfoeE

 
Said Salim Awadh Bakhresa.
KATI ya miaka ya 1960 hadi 1980, mtu kuwa tajiri alionekana ni hatari kwa taifa, tena mali zake alizimiliki kwa kificho, vinginevyo angeitwa mhujumu uchumi. Lakini kwa sasa mambo yamebadilika, taratibu sera za kibepari zinatawala, ujamaa unapewa kisogo.
Mtu kama ni mbunifu, ana nidhamu ya kutofuja pesa na anafanya kazi sana kwa nini asiwe tajiri? Utandawazi unasaidia ndiyo maana leo tunaweza kuwatambua mabilionea wakubwa ambao wanastahili

Sunday, September 1

Game Ya Liverpool Na Manchester United Na Game Ya Swansea Vs West Brom.
                           
NIENDE moja kwa moja kwenye  mada yetu ya leo ambapo tunaangalia kwa kina  jambo moja ambalo wanaume wengi wamekuwa  wakichukizwa nalo na kufikia hatua ya kusitisha suala la ndoa kwa watu waliotokea kuwapenda.
Wanawake wana hulka karibu sawa, kwa upande wa wanaume ni tofauti kidogo, wanaume wana hulka tofauti kulingana na matakwa na utashi wao, japokuwa kuna baadhi ya vitu huwa wanakaribiana sana hasa katika kutoa uamuzi!


Video tazama hapa:18 NL BOFYA HAPA


Kama unamfuatilia Jay Z kwa makini na wewe ni shabiki wake, Basi definitely utakuwa ume-note bonge moja la chain ambalo mkali huyu amekuwa akilitupia katika events mbalimbali,
-